Mnamo mwaka wa 2019, Mural Arts iliunda programu ya Same Day Work & Pay (Kazi na Malipo ya Siku Moja) ili kushughulikia upungufu wa watu wanaokabiliwa na ukosefu wa usalama wa kiuchumi. Mafanikio ya modeli hii yalipelekea Jiji la Philadelphia na mashirika mengine yasiyo ya faida kuunda fursa kama hizo. Same Day Work & Pay hutoa fursa za kazi zenye vikwazo vya chini hadi zile zisizo na vikwazo kwa watu wanaokabiliwa na ukosefu wa usalama wa kiuchumi, changamoto za afya ya akili na ya kitabia, na/au ukosefu wa makazi. Mpango huu pia hutoa huduma za kutoa msaada na njia ya kupata ajira ya kudumu.

Washiriki wa SDWP hufanya kazi ya kila siku ya saa 3.5 na kulipwa kati ya $50 na $100. Aina ya kazi inayofanywa inatofautiana kulingana na mshirika wa mwajiri.

Ofisi ya Uwezeshaji wa Jamii na Fursa (The Office of Community Empowerment and Opportunity) hutumika kama wakala ulio uti wa mgongo wa programu unaoangazia usawa wa rangi na uhamaji wa kiuchumi. Vizuizi vya kuajiriwa huathiri watu wa rangi tofauti, watu wanaokabiliwa na ukosefu wa uthabiti wa makazi, na wale ambao walikuwa gerezani hapo awali. Kuna washirika wanne wa ajira wanaoshiriki:

Mural Arts: Color Me Back

  • Maelezo ya programu: Urefu wa zamu ya chini ni saa 3.5. Zamu moja ni $50.
  • Maelezo ya kazi: Kupaka rangi michoro ya umma na miradi ya sanaa.
  • Vigezo vya kustahiki: Lazima uwe na angalau umri wa miaka 18 na uishi katika eneo la Philadelphia
  • Jinsi ya kutuma ombi: Tembelea https://bit.ly/colormeback

Community Life Improvement Program (CLIP), City of Philadelphia

  • Maelezo ya programu: Urefu wa zamu ya chini ni saa 3.5. Zamu moja ni $50.
  • Maelezo ya kazi: Urembeshaji na usafishaji wa jamii
  • Vigezo vya kustahiki: Lazima uwe na angalau umri wa miaka 18 na uishi katika eneo la Philadelphia
  • Jinsi ya kutuma ombi: Piga simu kwa 215-686-1550 (acha ujumbe wa sauti)

Uplift Solutions

  • Maelezo ya programu: Urefu wa zamu ya chini ni saa 3.5. Zamu moja ni $50.
  • Maelezo ya kazi: Uuzaji wa rejareja, ujenzi, matengenezo, na upishi
  • Vigezo vya kustahiki: Lazima uwe na angalau umri wa miaka 18 na uishi katika eneo la Philadelphia
  • Jinsi ya kutuma ombi: Tuma barua pepe kwa jeff.jones@upliftsolutions.org

Pennsylvania Horticultural Society

  • Maelezo ya programu: Urefu wa zamu ya chini ni saa 3.5. Zamu moja ni $100.
  • Maelezo ya kazi: Kutengeneza mazingira, usafishaji wa jamii
  • Ustahiki: Lazima uwe na angalau umri wa miaka 18, uishi katika eneo la Philadelphia, na uwe na kitambulisho
  • Jinsi ya kutuma ombi: Tembelea https://bit.ly/PHSworkphilly au piga simu kwa 215-988-8800, bonyeza 5
Jiunge na orodha yetu ya barua pepe ili upate maelezo zaidi kuhusu Same Day Work & Pay na programu zingine za wafanyakazi.